Stand United hatushuki daraja... Habari kamili soma matukio360 #share
BEKI wa kulia wa Stand United Aroun Michael (Mokoena) amewashusha presha mashabiki wa chama hilo lenye maskani yake mjini Shinyanga kuhusu kushuka daraja msimu ujao.
Stand United msimu huu wa Ligi kuu imeanza vibaya kwani mpaka sasa imecheza mechi tano na kufanikiwa kushinda moja huku nne ikipoteza.
Jambo hilo limefanya mashabiki kupata wasiwasi kwa timu yao kuwa inaweza kushuka daraja msimu ujao kutokana na matokeo hayo.
“Mashabiki wasife moyo ligi bado mbichi kabisa na kamwe hatuwezi kushuka daraja msimu ujao”alisema Mokoena.
Hata hivyo beki huyo aliwataka wachezaji wenzake kupambana kwani wanatakiwa kuanza kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ujao na Prison mjini Mbeya.
Stand ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama tatu ambapo jumamosi ya wiki hii itawavaa Prison katika mchezo utakaopigwa mkoani Mbeya.



No comments:
Post a Comment