UKAWA waanza tambo uchaguzi mdogo wa udiwani...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
VYAMA vya siasa nchini vilivyounda umoja ( Chini ya mwamvuli wa UKAWA) vipo katika hatua ya mwisho wa uratibu wa jinsi vitakavyogawana Kata 43 katika uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani, utakaofanyika Novemba 26, 2017.
Naibu mkurugenzi wa wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma-CUF Taifa, Mbarala Maharagande.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu. Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
Akizungumza na Matukio360 leo jijini Dar es Salaam Naibu mkurugenzi wa wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma-CUF Taifa, Mbarala Maharagande amesema uratibu wa ndani wa vyama (Kiutawala) unaendelea na maamuzi yatazingatia Utafiti wa Kisayansi unaoendelea kufanyika.
Awali tulieleza kuwa tungeweza kutoa msimamo wa mgawanyo wa Kata hizo Oktoba 11, 2017 lakini
Oktoba 23, 2017 imepangwa kufanyika kikao cha mrejesho wa hatua mbalimbali zilizofikiwa.
Amesema viongozi wa ngazi ya taifa watatoa tamko la pamoja kwa wakati muafaka kuonyesha mgombea wa chama kipi anapaswa kuungwa mkono katika kata husika.
Maharagande amesema hawatarajii viongozi wa Mikoa, Wilaya na Kata kwenda kinyume na maagizo ya ngazi za Taifa na wala hakutakuwa na visingizio vya aina yeyote ile vitakavyoleta MKANGANYIKO.



No comments:
Post a Comment