JPM amteua Janeth Masaburi...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Rais John Magufuli amemteua Janeth Masaburi kuwa Mbunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Janeth Masaburi
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Gerson Msigwa, imesema Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa
Ibara ya 66 (1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa
mamlaka ya kuteua wabunge 10 watakaokuwa miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Janeth Masaburi ataapishwa kulingana na taratibu za Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania

No comments:
Post a Comment