Kesi Malkia Pembe za Ndovu kusikilizwa mfululizo...soma habari kamili na Matukio360...#share
KESI ya uhujumu
uchumi ya meno ya tembo inayowakabili Salvius Matembo, Philemon Manase na raia
wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66) ya bilioni 13 kusikilizwa mfululizo kuanzia Oktoba 18,19 na 20,2017.
Meno ya Tembo
Wakili wa Serikali,
Paul Kadushi leo alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Huruma Shaidi kuwa kesi ilipaswa
kuendelea kusikilizwa Oktoba 17, 2017 na kwamba walimwita shahidi mmoja wa upande wa mashtaka lakini amepata udhuru.
Hivyo ameomba iendelee
kusikilizwa Oktoba 18,2017. Wakili wa
utetezi, Nehemiah Nkoko alieleza kuwa alitegemea upande wa Mashtaka
ungeandaa mashahidi wawili ama watatu, ili mmoja akipata udhuru wengine
waendelee.
Hivyo Hakimu Shaidi amewaambia upande wa Mashtaka
wazingatie hilo na kuiahirisha hadi
kesho itakapoendelea kwa ajili ya
usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa Mashtaka.
Washtakiwa wote
walikuwepo mahakamani pamoja na Mawakili wao wanaowatetea akiwamo Nehemia
Nkoko, Hassan Kihangio, Jeremiah Mtobesya.
Washtakiwa hao,
wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi,
2000 na Mei 22,2014 walijihusisha na
biashara ya nyara za serikali.
Katika kipindi hicho
washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo
vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na
Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Wanadaiwa kuwa kati
ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 kwa
makusudi raia wa China, China, Yang Feng Glan
aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha
vipande hivyo 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka
kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Kwa upande wa
washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa
kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno
ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.
Ilidai kuwa Mei 21,
2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase
alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo
Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za
nyara za serikali.




No comments:
Post a Comment