TAKUKURU yamvaa Mbunge Nassari...soma habari kamili na Matukio360...#share
Salha Mohamed
TAASISI ya Kudhibiti
na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imemuonya
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwamba aache kuishinikiza kufanya kazi na
kwamba itamchukulia hatua za kisheria.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari
Hatua hiyo inakuja
kufuatia hivi karibuni Joshua Nassari kuikabidhi
TAKUKURU ushahidi wake kwenye
flash na harddisk pamoja na nyaraka kadhaa kwa ajili ya ushahidi wa madiwani wa
Arusha kununuliwa na CCM.
Leo jijini Dar es
Salaam Mkurugenzi mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola amesema Nassari anapaswa
kuzingatia sheria bila kuathiri taarifa zake alizotoa.
“Endapo Mbunge
Nassari akiendelea na mwenendo huu hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Pia asiingize mambo haya kisiasa.” amesema Mlowola
Mlowola amesema kwa
mujibu wa sheria, inaitaka Takukuru imlinde mtoa taarifa lakini Nassari
amejitangaza hadharani kupitia vyombo vya
habari.
“Mbunge Nassari
anaendesha jambo hili kisiasa na si kisheria na kwa kuwa ameshaleta taarifa
zake, atuache tufanye kazi yetu.” amesema




No comments:
Post a Comment