Kesi mke bilionea Msuya kuunguruma Novemba..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
KESI
ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na
mfanyabiashara Revocatus Muyella itatajwa Novemba 13, 2017 baada ya jarada la
kesi kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI).
Mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita wa pili kutoka kulia akiwa Mahakamani
Wakili
wa Serikali, Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa
jalada halisi la kesi hiyo limetoka
ofisi ya upelelezi mkoa wa Temeke (RCO) na sasa lipo kwa DCI.
Kufuatia
maelezo hayo, Hakimu Simba amepanga kesi
hiyo kutajwa Novemba 13,2017 na amewasisitiza
upande wa Mashtaka kumaliza ushahidi wao mapema
Katika
kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2017, washtakiwa hao wanadaiwa kumuua kwa makusudi dada wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth
Msuya.
Tukio
hilo, linadaiwa kufanywa Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es
Salaam.
Washtakiwa
hao, awali Februari 23, 2016, waliachiwa
huru katika kesi ya mauaji namba 32 ya mwaka 2016 na Hakimu Mkazi Mwandamizi
Godfrey Mwambapa.
Baada
ya kufutwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikifanana na hii walikamatwa na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji
upya.
No comments:
Post a Comment