Shahidi kesi Malkia pemba za ndovu augua...soma habari kamili na Matukio360..#share

Na mwandishi wetu
SHAHIDI  upande wa mashtaka aliyetarajiwa kutoka ushahidi katika kesi inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan (66) ‘Malkia wa Pembe za Ndovu’ na wenzake wawili, anaumwa.

Baadhi ya pembe za ndovu
 Hayo yameelezwa leo na wakili wa serikali, Simon Wankyo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakam aya Kisutu, Huruma Shaidi.

Wankyo amedai   kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka na kwamba ushahidi waliyemtarajia atoe ushahidi anaumwa na hali yake bado siyo nzuri.

Hivyo ameomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa na wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko hakuwa na pingamizi.

Hakimu Shaidi ameahirisha hadi Novemba 7,2017 na kuamuru siku hiyo upande wa mashtaka upeleke mashahidi.

Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase ambao kwa pamoja, wanadaiwa kuwa  kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014  walijihusisha na biashara  ya nyara za serikali.

Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 13 bilioni  bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014  kwa makusudi raia wa China, China, Yang Feng Glan  aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.

Ilidai kuwa Mei 21, 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.





About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search