Kesi mke bilionea Msuya yanguruma... RTO Temeke atakiwa kufika Mahakamani...soma habari kamili na Matukio360...#share
KESI ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na
mfanyabiashara Revocatus Muyella imeendelea leo huku Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu ikiamuru mkuu wa upelelezi wa makosa
ya Jinai wa Temeke (RCO) afike mahakamani
hapo kueleza upelelezi umefikia wapi.
Mke wa marehemu bilionea Msuya,Miriam Mrita akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametoa agizo hilo leo wakati kesi hiyo ilipotajwa na kusisitiza ni lazima afike mwenyewe Oktoba 30,2017 bila ya kutoa udhuru.
Uamuzi huo umefuatia baada ya wakili wa Serikali, Patrick Mwita kuieleza
mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho kukamilika na
jalada lipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2017, washtakiwa hao wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth
Msuya.
Tukio hilo, linadaiwa kufanyika Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni
Jijini Dar es Salaam.
Februari 23, 2016 washitakiwa hao waliachiwa huru katika kesi ya mauaji namba 32
ya mwaka 2016 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mwambapa.
Baada ya kufutwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikifanana na hii
walikamatwa na baadaye kusomewa mashtaka
hayo ya mauaji upya.




No comments:
Post a Comment