Wapiga debe kuvaa sare...soma habari kamili na Matukio360...#share
SERIKALI Mkoani Mbeya imewaagiza wapiga debe
katika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani kuwa na sare zitakazowatambulisha ili kukabiliana na
matukio ya uharifu ikiwamo ukabaji, uporaji na utapeli.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla
"Wapiga debe wengi ni waharifu na wanatambuna tabia hizo sasa nawaagiza wachague uongozi, wawe na sare zitakazowatambulisha kisheria,” amesema
Mkuu wa mkoa huo Amos Makalla, ameimbia Matukio360 kuwa ni
wakati muafaka kwa wapiga debe kituoni hapo kuwa na sare za utambulisho wao.
Kituo hicho kimegharimu zaidi ya milioni 35.
Amesema utaratibu huo
ukifuatwa utapunguza kwa kiasi kikubwa
matukio mbalimbali ya kiharifu.
na kwamba wapigadebe hao wawafichue waharifu.
"Wapiga debe wengi ni waharifu na wanatambuna tabia hizo sasa nawaagiza wachague uongozi, wawe na sare zitakazowatambulisha kisheria,” amesema
Pia amewataka wafanyabishara kituoni hapo kuzingatia kanuni
za usafi ili kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwamo ugonjwa wa
kipindupindu.
Naye diwani
wa kata ya Sisimba Geofrey Kajigili (Chadema) ameiomba Serikali
kukarabati kituo cha polisi na ujenzi wa choo
kufuatia kuchakaa.
Amesema
kituo cha polisi hakina mazingira mazuri kiusalama na kwamba Serikali iweke mikakati ya kukiboresha.




No comments:
Post a Comment