Vigogo TIA waachiwa huru...soma habari kamili na Matukio360...#share



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo wawili wa zamani wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) baada ya kukamilisha masharti ya dhamana waliyopewa.



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Onesphor  na kaimu mtendaji wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Shaha Hanzuruni wameachiwa  na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kila mshtakiwa awe na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya milioni 250.



Pia  mdhamini mmoja kati ya wadhamini hao kuwasilisha fedha taslimu mahakamani milioni 250  ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha na kwamba mali hiyo ni lazima iwepo Dar es Salaam.



Masharti mengine ni  kila mshtakiwa  ametakiwa kusalimisha hati yake ya kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha Mahakama.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 24,2017. Washtakiwa hao  watasomewa maelezo ya awali

Wanakabiliwa na  mashtaka mawili likiwamo la matumizi mabaya ya madaraka na  kusababisha hasara ya Tsh 1,  097,681,107.



Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai akiwasomea hati ya mashtaka  washtakiwa hao amedai kuwa, kati ya Januari Mosi, 2012 na Desemba 30,2014 katika Chuo cha Uhasibu Tanzania kwa nafasi zao, walitumia madaraka vibaya kwa kutofuata taratibu za ununuzi katika kununua ardhi ya kampasi ya Chuo cha TIA Mwanza.

Amedai kuwa kitendo hicho kilisababisha Vedastus Ngasa Lukago kupata manufaa ya Tsh 1, 097, 681,107.

Swai amedai kuwa,  katika kipindi hicho cha Januari Mosi,2012 na Desemba 30,2014 washtakiwa hao wakiwa waajiliwa wa Chuo hicho, kwa ridhaa na kwamatendo yao walisababisha hasara ya Tsh 1, 097,681,107.

Fedha ambayo ni Mali ya Chuo cha Uhasibu Tanzania kutokana na kutokufuata taratibu za manunuzi wakati wa kusaini mkataba wa ununuzi wa ardhi ya Chuo Cha Uhasibu Tanzania kampasi ya Mwanza.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.












About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search