Kesi mtandaoni ya ACACIA yanguruma...soma habari kamili na Matukio360...#share
UPELELEZI wa
kesi ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Face book kuhusu mazungumzo kati ya
Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia, inayomkabili mkazi wa Chato
Geita, Obadia Kiko (41), katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haujakamilika.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Hayo
yameelezwa jana na Wakili wa Serikali, Adolf Mkini kwa Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Baada ya
kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba
14,2017 kwa ajili ya kutajwa.
Katika kesi
hiyo, mshtakiwa anadaiwa Agosti 3,2017 huko Chato Geita alifanya kosa hilo
kupitia mtandao wa Face book.
Mshtakiwa
anadaiwa kusambaza maneno kuwa " Taarifa kutoka kikao cha mazungumzo kati
ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu
wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada
kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni hivi ni vituko mwizi anakusaidia sheria
haahaa haha."
Inadaiwa
aliendelea kusambaza maneno kuwa "Mazungumzo bado yanaendelea lakini
wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo vyote vya
mikataba kiukweli tumuombe mungu maana Serikali ikitaka kuvunja mkataba na
Acacia gharama kubwa zitatuhusu."
"Lakini
pia kuendeleza uvyama utatugharimu saana,
baada ya mh. Rais Magufuli angewashirikisha Mawakili wasomi
waliokwishaiva wakili Lissu, wakili Kibatara na Fatma Karume kwenye mambo ya
umuhimu kama haya yeye kaleta uchama sasa itatugharimu .// Dicteta Magufuli
mist go" . Maneno hayo yanadaiwa kusambazwa na mshtakiwa huyo kupitia
mtandao huo wa kijamii wa Facebook.
Imedaiwa
maneno hayo yalikuwa na lengo la kupotosha umma. Mshtakiwa amekana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana.




No comments:
Post a Comment