Maiti zaendelea kuopolewa Somalia...soma habari kamili na matukio360...#share
MIILI ya watu
waliouawa kwenye mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi
kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imeendelea kuopolewa huku miili 160 ikizikwa jana na serikali kutokana na kutotambulika.
Mwili ukiopolewa kutoka katika moja ya jengo lililovunjika kutokana na milipuko ya mabomu Mogadishu Somalia
Inadaiwa idadi ya
waliokufa hadi sasa imefikia zaidi ya watu 300, kwa mujibu wa ripoti ya shirika
la habari la Reuters na kwamba takriban watu wengine 300 wamejeruhiwa kwa
mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa vilipuzi lilipolipuka karibu na
lango la hoteli.
Ahmed Ali ambaye ni mwuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja mbali
na miili 160 iliyozikwa na serikali miili mingine ilizikwa na jamaa zao.
Hilo ndilo shambulizi
baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati
zake mwaka 2007.
Rais Mohamed
Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa
shambulizi hilo katili.
Rais huyo alichangia
damu na tayari Uturuki imefungua kambi kubwa ya
kijeshi Somalia
"Tumethibitisha
kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idadi ya waliokufa huenda bado
ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir
Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia
shiria la Reuters.




No comments:
Post a Comment