Kesi ya vigogo wa Wizara Nishati, Madini yaunguruma..Soma habari kamili na Matukio360..#share
UPELELEZI wa kesi inayomkabali mthamini wa madini ya Almas wa serikali,
Edward Joseph Rweyemamu(50) na Mkurugenzi wa tathimini, Archard Alphonce
Kalugendo(49) umekamilika kwa kiasi kikubwa.

Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na
Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) wakitoka
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon
ameeleza hayo leo kwa Hakimu Mwandamizi,
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Godfrey Mwambapa wakati kesi hiyo
ilipotajwa.
Wakili Wankyo amedai upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na
wamewaelekeza polisi kufanya upelelezi na tayari sehemu kubwa ya upeleleze
umekamilika.
Amedai kutokana na hali hiyo,
tarehe ijayo wataieleza Mahakama upelelezi huo
umefikia hatua gani.
Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi
hiyo hadi Oktoba 26,2017.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na
kesi ya uhujumu uchumi kwa kusababisha
hasara ya dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.
Kalugendo ambaye ni mkazi wa
Kinyerezi na Rweyemamu mkazi wa Mwananyamala wote ni waajiriwa wa wizara ya
Nishati na Madini.
Kati ya Agosti 25 na ,31, 2017
katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa hao kwa
pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati
na Madini walisababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Baada ya kusomewa shtaka hilo,
washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu
haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Washtakiwa wapo
rumande.




No comments:
Post a Comment