Masogange kuanza kujitetea kesi ya dawa za kulevya..Soma habari kamili na Matukio360..#share
MSANII maarufu wa unogeshaji wa
video (Video Queen) Agnes Gerald(Masogange) ataanza kujitetea katika kesi
inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya Novemba 14, 2017.
Video Queen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akizungumza na wakili Rouben Semwanza leo mara baada ya kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam .
Mshtakiwa huyo alipaswa kuanza kujitetea
leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba kwa
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ipangiwe tarehe nyingine.
Kufuatia maelezo hayo, Hakimu
Mashauri ameiahirisha hadi Novemba 14, 2017 ambapo ataanza kutoa utetezi wake.
Pia hatua hiyo imefikiwa baada ya
Hakimu Mashauri kumuona mshtakiwa Masogange
ana kesi ya kujibu na anapaswa kujitetea na kuwaita mashahidi ambao ni watatu.
Masogane anatetewa na
Mawakili Nehemia Nkoko na Ruben
Simwanza.
Kesi hiyo inaendeshwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula na
wanamashahidi watatu
Masogange anakabiliwa na mashtaka
mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Anadaiwa kufanya makosa hayo
chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa za kulevya namba 5
ya mwaka 2015.
Katika kesi hiyo namba 77 ya
mwaka 2017, Masogange anadaiwa kati ya
Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es
Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya
Heroin (Diacety Imophine).
Pia anadaiwa kuwa kati ya
Februari 7 na 14,2017 alitumia dawa za
kulevya aina ya Oxazepam.
Video QUeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri ya matumizi ya Dawa za kulevya na kesi yake kupigwa Kalenda mpaka Novemba 14, 2017.



No comments:
Post a Comment