Liverpool, Man U hakuna mbabe... habari kamili soma Matukio360..#share


TIMU ya soka ya Liverpool na Manchester United zimetosha nguvu baada ya kwenda sare ya bila kufungana.

Kipa wa Man U, David De Gea akiokoa  mpira katika mechi na Liverpool
Mchezo huo liochezwa katika uwanja wa Anfield kwa sehemu kubwa ulitawaliwa na Liverpool  kwa kulishambulia lango la Man U ambao kwa muda mwingi walikuwa wakizuia.

Kufuatia mechi hiyo Man u imefikisha pointi 20 katika mechi nane iliyocheza huku Liverpool ikifikisha pointi 13.

Klabu hizo mbili ni mahasimu wakuu mashabiki wa timu hizo wanauadui wa kihistoria.

Katika mpambano huo Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa akiadhimisha miaka miwili tangu atue Liverpool

Katika mechi hiyo Liverpool ilimkosa mchezaji wake tegemeo Sadio Mane aliyeumia misuli ya paja akichezea Senegal mechi za kufuzu Kombe la Dunia lakini Klopp anaamini wanaweza kujimudu bila yeye.

Mane anatarajiwa kukaa nje wiki sita.

United walimkosa kiungo wa kati  Marouane Fellaini  kutokana na kuumia kano za goti akichezea Ubelgiji. Pia na nahodha Michael Carrick ambaye bado anauguza jeraha

Wachezaji wengi wa timu mbalimbali wametoka kuchezea timu za taifa na majeraha - ni tatizo kubwa kutokana na mabadiliko ya mtindo wa mazoezi na uchezaji pia.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search