Rais Magufuli ampiga kijembe Maalim Seif... Kuingiza bilioni 159 aokoa bilioni 86...soma habari kamili na Matukio360...#share
NDIVYO unavyoweza kusema hicho ni kijembe kufuatia rais
wa Tanzania Dk John Magufuli kushangazwa
na kauli kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif ataapishwa kuwa rais wa
Zanzibar.
Rais Dk John Magufuli akimsikiliza kwa makini rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassani Mwinyi
“Hivi karibuni wapo wengine wamejitapa wataapishwa eti
kuwa rais wa Zanzibar lakini mbona hadi sasa ajaapishwa.”
Rais Magufuli amesema hayo leo mjini Zanzibar
alipokuwa akihutubia katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 18 ya kifo cha
rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julias Nyerere, kilele cha mbio za mwenge
na siku ya vijana kitaifa
Pia amesema katika mwezi ujao serikali itaingiza zaidi ya bilioni 159 kwa ajili ya
mishahara na malupulupu kwa wafanyakazi wa serikali na kwamba imeokoa zaidi ya
bilioni 86 ambazo zingelipwa kwa wafanyakazi hewa.
Amesema si kwamba
hataki kuongeza mishahara na kwamba hilo linategemeana na hali halisi ya
mahitaji ya nchi kwa wakati husika.
“Si kwamba sitaki kuongeza mishahara na malupulupu ila
ni vigumu kutekeleza hilo wakati nchi inahitaji kufanya mambo mengi ya kusaidia
watanzania. Pia upo uwezekano huo,” amesema na kuongeza
“Mwezi ujao serikali itaingiza zaidi ya bilioni 159
katika mishahara na imeokoa zaidi bilioni 86 ambazo zingelipwa kwa wafanyakazi hewa.”
Hata hivyo, Rais Magufuli amesema halizishwi na
mashinikizo yanayotolewa na wadau mbalimbali kuhusu ongezeko la mishahara na
malupulupu.
“Kusiwepo na shinikizo la kulazimisha kudai ongezeko
la mishahara na malupulupu.” amesema
Hivi karibuni kumekuwapo na taarifa inayomuhisisha
katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa anadai ataapishwa kuwa rais
wa Zanzibar.




No comments:
Post a Comment