Lowasa ampokea Nyalandu CHADEMA, LHRC wampongeza...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
MJUMBE wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha Lazaro Nyalandu katika chama hicho huku kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kikiunga mkono hoja za
kujivua Ubunge na kuachia nyazifa zote ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Nyalandu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, Lazaro
Nyalandu.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Hellen Kijo Bisimba.
Mapema leo Nyalandu ametangaza
kuchukua hatua hiyo kwa kile anachodai kuwa hali ya sasa ya kisiasa nchini siyo
nzuri kutokana na kuwepo ukandamizaji wa
Demokrasia kwa kuminya uhuru wa kijeleza na kutoa maoni pamoja na matendo
yanayoashiria uvunjifu wa Katiba .
Akizungumza leo na Matukio360
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Hellen Kijo Bisimba, amesema kitendo cha
Nyalandu kuhama CCM ni haki yake ya Kikatiba
na kueleza kuwa sababu alizotoa za kuhama ni za msingi kutokana nchi kupitia
kwenye kipindi kigumu katika masula ya Demokrasia.
Aidha amesema kwa sasa kitendo cha Nyalandu kuibuka na kusema
hadharani ni ishara ya kuchoka kukishauri chama
hicho bila kusikilizwa hivyo akaamua kujiandoa mwenyewe na kusema
hadharani .
“Nyalandu anahaki kama raia ya
kufanya uchambuzi wa masuala
yanayoendelea, sisi kama watetezi wa haki za binadamu tunaweza kukubaliana naye
kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ukandamizaji ikiwemo kutokuwepo na haki ya kujieleza, akiwa ndani ya CCM amefanya
uchambuzi ameyaona hayafai” amesema Dk. Bisimba.
Ameongeza kuwa uongozi wa kipindi
kilichopita wa Serikali ya CCM ulikuwa
ukitoa uhuru wa kujieleza na kuruhusu wananchi kuikosoa lakini kwa sasa hali
imebadilika.
“Tumezoea miaka iliyopita uhuru
ulikuwepo,lakini sahivi licha ya kuwepo kwa Haki za binadamu lakini kumekuwepo
kwa sheria kandamizi ikiwemo sheria ya mtandao,leo uhuru wa Kikatiba wa
kukusanyika umeminywa,Tunashuhudia Wabunge wakikamatwa”
“Kwa mfano tumeshuhudia mbunge wetu
wa Kawe (Halima Mdee) amekamatwa kwa amri ya mkuu wa Wilaya na hata Rais
anashindwa kumchukulia hatua Mkuu huyo wa Wilaya “ amesema Dkt Bisimba.
Dkt Bisimba amewataka wanajamii
kutobeza uamuzi wa Nyalandu kwani ni haki yake Kikatiba.
Naye Lowassa amemkaribisha kwa mikono miwili Nyalandu na kwamba Chadema ndio mahala panapomfaa
Naye Lowassa amemkaribisha kwa mikono miwili Nyalandu na kwamba Chadema ndio mahala panapomfaa
No comments:
Post a Comment