Wa-Iran kumi, Watz wawili wa dawa za Heroin wapandishwa kizimbani..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
Wa-Iran kumi na Watanzania
wawili leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na
mashtaka matatu ikiwamo la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin
kilo 111.02
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Victoria Nongwa kuwa Oktoba 25, 2017 watuhumiwa hao walikutwa katika ukanda wa
bahari ya Hindi upande wa Tanzania wakisafirisha kilo 111.02 za Heroin na
bangi gramu 235.78
Imedaiwa siku hiyo
washtakiwa hao walichanganya dawa za kulevya aina ya Bangi na Kuberi zenye uzito
wa kilo 3.34.
Baada ya kusomewa mashtaka
hayo washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo
haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo. Walikuwa wakitafsiriwa lugha ya
kiswahili kwenda Kiirani na mkalimani Meja Ndakeye (45)
Upande wa mashtaka
umedai upelelezi bado haujakamilika na
washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Novemba 13,2017 itakapotajwa.
Hata hivyo kutokana
na kiwango cha dawa kuwa kikubwa mahakama
ya Kisutu haina mamlaka kutoa dhamana kwa washtakiwa hao.
Washtakiwa hao ni
Nabibakshsh Bibarde40, Mohammed Dorzade (23), Abdallah Sahib, Ubeidulla Abdi,
Naim Ishaqa, Moslem Amiree, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Tahir Mubarak, Abdulmajid Asqan, Ally
Abdallah na Juma Juma.
No comments:
Post a Comment