Lulu aeleza Kanumba alivyofariki.. soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
MUIGIZAJI
wa maigizo Elizabeth Michael 'Lulu' amesimulia
namna kifo cha mpenzi wake, Steven Kanumba kilivyotokea huku akieleza Mahakama hajasababisha kifo hicho na kwamba yeye ndiye
angekuwa marehemu kwa sababu ya kupigwa na panga.
Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akiwa mahakamani
Akiwa
ni mwenye simanzi Lulu ameileza Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa hajahusika kwa namna yoyote kwenye kifo cha
marehemu Kanumba
Lulu
ambaye amebainisha wazi kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa miezi minne
na Kanumba kabla ya kifo chake, alikuwa akienda mara kwa mara nyumbani kwake na
kwamba walikuwa wanaficha mahusiano yao ili kukwepa mitandao ya kijamii na
vyombo vya habari.
Akiongozwa
na Wakili wake, Peter Kibatala, Lulu alidai mbele ya Jaji Sam Rumanyika kuwa Aprili 6, 2012
alikuwa nyumbani kwao Tabata na jioni alitaka kwenda kwa marafiki zake
Mikocheni kwa ajili ya kwenda klabu.
Alidai
walikuwa wakiwasiliana na marehemu Kanumba kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi
licha ya kwamba hakutaka kumwambia kama anataka kutoka na marafiki zake kwa
sababu alikuwa hapendi atoke.
"Marehemu
alikuwa akinipigia simu mara nyingi kujua nipo wapi ndipo nilimwambia kuwa
nataka kutoka ili asinisumbue nikamueleza kuwa nitapita nyumbani kwake kumuaga
lakini sitokaa sana. Kabla ya kufika alinipigia na kunambia kuwa ataacha mlango
wazi hivyo nipite mpaka chumbani..nyumba niliizoea hata asipokuwepo nilikuwa
naenda," alidai Lulu.
Aliendelea
kudai kuwa alimkuta Kanumba chumbani akiwa na taulo huku akipaka mafuta
kichwani ambapo yeye alikaa kitandani na kusalimiana.
"Kama
tunavyojua marehemu alikuwa anajipenda sana hivyo alikuwa ameweka superblack
kwenye nywele zake na kwamba alikuwa na mafuta maalum ili zing'ae.
Tulisalimiana
na muda kidogo simu yake iliita na alipokea alikuwa ni Chaz Baba akamwambia anakuja. Wakati huo alikuwa
anakunywa pombe aina ya Jack Daniel na Sprite na ameshaanza kulewa,"
alidai.
Pia
alieleza kwa kuwa marehemu Kanumba alikuwa hapendi atoke, alimtaka waende
sehemu moja ambapo mara nyingi akilewa huwa
anampiga hivyo hakutaka kumbishia kutoka naye.
Lulu
alidai hupendelea kwenda disco wakati marehemu Kanumba alikuwa anapenda kwenda
kwenye bendi ambazo alidai kwake ni za
kizee wakati huo aliwaahidi marafiki zake kuwa atarudi.
Alidai
baadae marafiki zake walianza kumpigia kumuuliza ulipo ambapo aliogopa kupokea
simu mbele ya Kanumba kukwepa kuulizwa
anakwenda wapi hivyo alimuaga na kumueleza kuwa anakwenda kuchukua maji
jikoni na alipofika kwenye korido
Kanumba alimfuatilia kwa nyuma na kumuuliza anaongea na nani.
"Nilijua
utani huku nikiwa nacheka nikamjibu kuwa naongea na rafiki yangu kwa sababu
nilizoea anapenda kujua naongea na nani
lakini baadae nilianza kuogopa baada ya kuona sura yake imebadilika
hivyo nikawa natoka nje naye alianza kunifuata na hii sio mara ya kwanza
kunipiga na hufanya hivi akiwa amelewa maana hata mtu alinipigia au kumkumbatia
alikuwa hapendi," alieleza na kuongeza;
"Nilikimbia
hadi nje wakati huo marehemu alikuwa na taulo hivyo nikadhani kwamba ataona
aibu kutoka nje hivyo huku akiwa kifua wazi lakini alinifuata hadi nje umbali
wa hatua 28 lakini aliendelea kunikimbiza hadi getini akatoka nje ya geti
ambapo kuna barabara ya Sinza Kijiweni na Tandale..tuliendelea kukimbizana hadi
nikajificha lakini aliniona na kunipiga vibao na kunifunga mikono yangu kwa
mkono wake mmoja."
Muigizaji
huyo pia alidai Kanumba alianza kumpiga mateke na kumburuza huku akiwa na taulo
lake na kwamba mdogo wake, Seth Bosco alikuwepo lakini hakutoka kumsaidia.
Alidai
baada ya kuburuzwa alinyanyuka na alipelekwa moja kwa moja hadi chumbani na
mlango ulifungwa kwa funguo kwa ndani na kutupwa kitandani kwa sababu alihisi
simu aliyokuwa anaongea naye ni mwanaume mwengine.
Lulu
alidai marehemu Kanumba alitoa panga na kwa sababu walikimbia alikuwa anahema
sana na kumwambia kuwa atamuua hivyo alianza kumpiga kwa mabapa ya panga kwenye
mapaja naye alikuwa akikinga asikatwe usoni.
Vile
vile, alidai Kanumba alikuwa anapumua
kwa kasi na kutupa panga chini na kuwa kama mtu anayekabwa baadae alinguka na
kujigonga kwenye ukuta muda huo yeye alikuwa kitandani.
"Alipokuwa
anataka kuamka nilihisi anataka kunifuata tena nikitoka nikajifungia chooni
wakati huo yeye alianza kutapatapa.
Nilijaribu kupiga kelele kupata msaada lakini hakuna baadaye nilisikia kishindo
cha mtu kuanguka au mlango uliobamizwa na kusikia ukimya. Sikuwa za kama ameanguka
nilihisi hasira zake tu kwani nilipofungua mlango wa bafuni nilimkuta amelala na wakati huo
kulikuwa na mwanga wa mshumaa kwani umeme ulikatika," alidai.
Lulu
alidai kwa akili zake aliwaza kuwa Kanumba amwjifanyisha kuzimia ili isiwe
tatizo kwake ambapo alianza kumwambia kuwa hata mtu akija atamwambia kila kitu
kilichotokea lakini akawa hajibiwi.
Alidai
alichukua maji chooni na kumgusisha machoni kuona kama ataamka na baadaye
alifungua mpango na kumuita Seth na kumueleza kuwa Kanumba ameanguka ambaye
naye alijaribu kumuacha lakini hakuamka na kumpigia simu daktari wake.
Lulu
anasimulia kuwa alimwambia Seth hawezi kubaki nyumbani hapo badala yake akitoa
naye atatoka kwani akiamka atamuua hivyo
aliondoka na gari hadi Coco beach.
Aliendelea
kudai kuwa alimpigia simu daktari wa familia Paplas ambaye alikuwa anajua mahusiano yao na wakati
akiumwa alikuwa anamtibu na kwamba alimueleza kuwa rafiki yake amempiga sana na
iwe mara ya mwisho kutafuta kwa sababu alimshikia panga na siku nyingine
atamuua.
Alieleza
kuwa alikuwa haruhusiwi kutoka nyumbani kwao usiku hivyo alikuwa anabeba nguo
za ziada na anaporudi nyumbani asubuhi hudanganya kama alitoka kuosha vyombo wakati
anatokea klabu.
"Nilipokea
simu nyingi kuniuliza kama kweli Kanumba amekufa nilimpigia simu Seth ambapo
alikuwa hapokei nilimpigia Dk Paplas akamuuliza kuhusu masuala ya nyumbani
imekuwaje kwa sababu amepigiwa simu kuuliza ambaye akamwambia kuwa hajafa ila
wapo hospitali na kukata simu. Baadaye Dk Paplas alinipigia kuniuliza niko wapi
tukutane," alidai
"Kwa
sababu nilijua Kanumba na huyu daktari ni marafiki, nilijua anamtumia rafiki
yake waweze kukutana tena mara ya kwanza
nilimkatalia ya kwanza na nikamuuliza kama amezidiwa yupo hospitali gani
niende. Nilitaka anihakikishie alipo na asije na Kanumba na wala hakunambia
kama ameshakufa," alieleza Lulu.
Alidai
walikutana Bamaga na Dk Paplas na ndipo askari walimkamata bila ya kumwambia
sababu na walipofika Kituo cha Polisi, Oysterbay Polisi akakutana na watu wengi
ikiwemo msanii Vincent Kigosi 'Ray' na kuhisi kwamba Kanumba amekamatwa.
Alidai
alichukuliwa maelezo na kuonesha sehemu alizojeruhiwa kwa kipigo na askari wa
kike ndiye aliyethibitisha na kwamba alichukuliwa maelezo mara nne ambapo
alipata taarifa za kifo cha Kanumba akiwa selo.
Siku
inayofuata, Lulu alidai alimueleza Afande Ernatus kwamba anaumwa hivyo
alipelekwa hospitali ya Mwananyamala akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na
kuandikiwa dawa.
"Sijasababisha
kifo chake yeye ndiyo alikuwa ananishambulia kwa silaha pengine asingeanguka
mimi ndio ningekuwa marehemu kwa sababu sikuwa na njia yoyote ya kujitetea kwa
sababu ya umbile langu dogo," alidai Lulu.
Hata
hivyo, Jaji Rumanyika alimtaka Lulu kueleza kama wakati huo anaendesha gari
alikuwa na leseni ambapo alidai kuwa hakuwa nayo mpaka baada ya matatizo hayo
ndio aliomba leseni.
Kabla
ya Lulu kuanza kujitetea Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya
binadamu na vifo vyenye utata kutoka Hospital ya Taifa ya Muhimbili, ambaye pia
ni shahidi wa mwisho upande wa Jamuhuri, Inocent Mosha ameileza Mahakama kuwa mwili wa Marehemu Kanumba ulikatwa
vipande vipande na kupelekwa kwa mkemia kwa uchunguz zaidi
Alieleza
kuwa walichukua kipande cha utumbo, chakula kilichomo, kipande cha ini, figo,
mkojo, damu, mamji maji kwenye jocho na kucha.
Akiongozwa na wakili wa serikali Faraja George shahidi
huyo alisema Aprili 9,2012 akiwa Muhimbili alipokea amri halali ya polisi
ikiamuru kufanya uchunguzi wa Mwili wa Kanumba uliokuwa umehifadhiwa chumba cha
kuhigadhia maiti.
Alieleza
kuwa wakati wa uchunguzi huo walikuwa na mashahidi wawili walisaidia kutambua
mwili wa marehemu ambapo walianza kuangalia kama ana majera ya nje ya mwili.
"Tuliangalia
kwenye kucha zake za vidole zilikua na rangi ya buluu, pia tulifungua viuonga
vya ndani vya mwili ambapo kwenye kisogo kulikuwa na mvilio wa damu. Tulifungua
fuvu la kichwa na kuona ubongo umevimba"alidai.
Aliendelea
kudai kwenye mishipa midogo iliyokuwemo kwenye ubongo inayosambaza damu
ilivilia damu na sehemu ya chini ya ubongo kulikuwa na mkandamizo wa damu
Alieleza
kuwa walifungua mapafu,moyo, figo, maini, tumbo na mifumo mingine ya mwili
haikuwa na tatizo.
Shahidi
huyo alidai katika ripoti yake aliyoiandaa kwenda kwa mkemia, ilionesha kuwa
anatatizo kwenye mfumo wa upumuaji ambapo ulishindwa kufanya kazi kutokana na
majeraha kwenye ubongo.
"Hakuwa
na majeraha kwa nje lakini mapafu yalijaa damu ambapo tulikata kucha kufanya
vina saba, tulichukua majimaji ya kwenye jicho kuangalia kiasi cha pombe na
sukali kwenye mwili" alidai
Pia
alidai kuwa pombe haiwezi kusababisha matatizo hayo moja kwa moja badala yake mabadiliko ya tabia yanayotokan
na unywaji ndio yanaweza kuchangia.
Alipoulizwa
swali na wakili wa utetezi Peter Kibatala shahidi alisema hatambui kama seth
Bosco alikuwepo wakati wa uchunguzi kwa sababu sio lazima mtu kuwepo mwanzo
mwisho.
Alieleza
kuwa hafahamu kiwango cha pombe na hafahamu kama alijigonga kwasababu ya pombe
na kwamba hawakuchukua sampuli ya ubongo.
Keshi
hiyo imeahirishwa mpaka kesho ambapo upande wa utetezi utakuwa na shahidi mmoja
Josephine Mushumbus ambaye wanadai kuwa yupo nje ya nchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment