Tanzania yazidi kuporomoka Duniani...soma habari kamili na Matukio360..#share
Shirikisho la
soka duniani Fifa limetoa orodha mpya ya viwango vya soka duniani baada ya
kuchezwa kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018, Kenya na Tanzania
zikishuka zaidi ya hatua 10 kwenye orodha hiyo..
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta
Ujerumani bado
wanaongoza wakifuatwa na Brazil na Ureno.
Tanzania
inashikilia nafasi ya 136 sasa baada ya kushuka nafasi 11, Kenya nayo imeshuka
nafasi 14 hadi nafasi 102.
Katika mechi
za kirafiki ambazo Harambee Stars walicheza hivi majuzi, walilazwa 1-0 na
Thailand baada ya kuchapwa 2-1 na Iraq mjini Basra.
Burundi
imesalia nafasi ya 129, Uganda ikapanda hatua moja hadi nafasi ya 70.
Malawi
imeshuka nafasi moja hadi nambari 117 ambapo inafuatwa katika nafasi ya 118 na
Rwanda ambao bado walishikilia nafasi hiyo katika orodha iliyotangazwa awali.
DR Congo
wamepanda nafasi 7 hadi nafasi ya 35.
Afrika Tunisia
wanaongoza kiwa nafasi ya 28 duniani baada ya kupanda hatua 3 wakifuatwa na
Misri walio nafasi ya 30 duniani
Orodha ya Fifa
Nafasi Taifa
1 Ujerumani
2 Brazil
3 Ureno
4 Argentina
5 Ubelgiji
6 Poland
7 Ufaransa
8 Uhispania
9 Chile
10 Peru
11 Uswizi
12 England
13 Colombia
14 Wales
15 Italia
16 Mexico
17 Uruguay
18 Croatia
19 Denmark
20 Uholanzi




No comments:
Post a Comment