Makamu wa Rais awasili Mkoani Kilimanjaro...Soma habari kamili na Matukio360..#share

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewasili Mkoani Kilimanjaro ambapo anatarajiwa kesho kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama kitaifa.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Alipowasili mkoani humo amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa huo Anna Mghwira pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.




Ufunguzi huo utafanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo katika Manispaa ya mji wa Moshi na Kauli mbiu ya mwaka huu ni ” Zuia Ajali-Tii Sheria Okoa Maisha”








About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search