Mbeya kutoa asilimia 10 ya mapato kwa wanawake na vijana..Soma habari kamili na Matukio360..#share
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, ameagiza halmashauri zote
kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake na vijana ili kutekeleza lengo la
serikali kuwezesha makundi hayo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla
Akizungumza na Matukio360 Makalla amesema ameziagiza halmashauri kutoa fedha hizo.
"Tayari nimeagiza halmashauri zote kuhahakisha fedha zinatolewa kwa wakati na si kwa kificho na
kwamba vyombo vya habari vishirikishwe,"amesema
Aidha amesema katika halmashauri saba za mkoani Mbeya, halmashauri
ya chunya inaongoza kimkoa na kitaifa kwa utoaji wa mikopo kwa wanawake na
vijana huku jiji la mbeya likishika mkia
Awali mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chunya Sophia
Kumbuli amesema mwaka 2016/17 imetolewa mikopo ya zaidi milioni 300 kwa wanawake na vijana katika mapato yake ya
ndani



No comments:
Post a Comment