Naibu Waziri Mabula atoa siku 90 kwa Ofisa Ardhi Hanang...Soma habari kamili na Matukio360..#share
NAIBU Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabulla ametoa siku 90 kwa Ofisa
Ardhi Mteule wa Halmashauri ya wilaya ya Hannang mkoani Manyara, Egidius
Kashaga kurekebisha mfumo wa uhifadhi wa hati za umiliki ardhi.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabulla
akipekua mafaili ya kuhifadhia hatimiliki za ardhi wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza katika idara ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Hannang na kukuta
mfumo mbovu wa uhifadhi wa hati za kumiliki ardhi hali ambayo ni rahisi kwa
maafisa hao kudanganya na kumilikisha mtu zaidi ya mmoja.
Imebainika
kuwa mifumo hiyo inamapungufu ambayo ni rahisi kwa maofisa hao kudanganya na
kumilikisha ardhi kwa watu zaidi ya mmoja.
Mabula
ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika idara ya ardhi
ya halmashauri ya wilaya hiyo.
“Nakupa
siku 90 uwe umerekebisha huu mfumo, na kama ndani ya kipindi hiki utashindwa kutekeleza
agizo hilo nitakuvua cheo chako na kukuadhibu kwa mujibu wa sharia,” amesema
Mabula.
Wakati
wa ziara hiyo Mabulla ameamua kupekua Hati za mwananchi mmojammoja na kugundua
baadhi ya hati hizo hazina vielelezo vya kumbukumbu na baadhi ya nyaraka za umiliki
wa ardhi hazina mtiririko mzuri wa uhifadhi wa mafaili.
Katika
hatua nyingine Mabulla amekutana na wananchi wa Kata ya Mogitu, Wilaya humo na
kusikiliza kero zao za ardhi hasa suala la muwekezaji wa Kiwanda cha Manyara
Cement Limited ambaye ameomba eneo la ujenzi wa kiwanda la ukubwa wa ekari 370.
Mmiliki
huyo James Mtei alipeleka maombi yake kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hannang
akiomba ardhi katika kijiji cha Mogitu
ili ihawilishwe na imilikishwe kwa Kampuni yake kwa hati miliki chini ya Sheria
ya Ardhi (Sura 113) kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji saruji.
Mabulla
ametembelea eneo hilo linalotaraji kujengwa Kiwanda cha uzalishaji saruji ili
aweze kujiridhisha kabla ya kummilikisha mwekezaji huyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mheshimiwa Dk. Angeline Mabulla akiongea na wananchi wa Kata ya Mogitu, Wilaya
ya Hanang mkoani Manyara mara baada ya kusikiliza kero zao za ardhi hasa suala
la muwekezaji wa Kiwanda cha Manyara Cement Limited ambacho kimeomba eneo la
ujenzi wa kiwanda la ukubwa wa ekari 370.



No comments:
Post a Comment