Mhasibu Wa Shule Atiwa Hatiani Kwa Kosa hili Dhidi ya JPM...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

MHASIBU wa Shule ya Sekondari St Joseph, Elizabeth Asenga ametiwa hatiani kwa kosa la kumuita Rais John Magufuli kilaza.
Elizabeth ametiwa hatiani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa jamhuri kuthibitisha kosa.

Mhasibu huyi anadaiwa kuandika “hakuna rais kilaza kama yeye duaniani” katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Hakimu Shaidi akitoa uamuzi wa mahakama, alimtaka mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh milioni tano au jela mwaka mmoja ambapo amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search