RC Rukwa asifu juhudi zinazofanywa na TAWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Steve Zelote (Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi) amekutana na uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania - TAWA ofisini kwake Mjini Sumbawanga.
Akiongoza mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  TAWA Dkt. Wakibara amewataka watumishi wa pori la Lwafi kufanya kazi kwa bidii na kutojiusisha na vitendo vya rushwa.
Nae Mkuu wa Mkoa amesifu juhudi zinazofanywa na askari wanyamapori kutoka mapori ya Akiba Uwanda na Lwafi Mkoani Rukwa, hasa suala la kuondoa ng'ombe Ndani Ya hifadhi.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amemuomba Dkt. Wakibara kusaidia operesheni za kuondoa mifugo katika wilaya zote za Mkoa wake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu. TAWA yuko katika ziara yake ya kutembelea Mapori Akiba(Game Reserves). Baada ya safari yake ya kutoka Mkoa wa Katavi na Rukwa ataendelea Mkoa wa Singida na Mbeya kutembelea Pori la Rungwa/Kizigo/Muhesi liliopo katika mikoa hii miwili ili aweze kuongea na watumishi wa mapori hayo na kusikiliza changamoto mbalimbali za utendaji kazi na kujadiliana nao kuona uwezekano wa kuzitatua

Picha ya pamoja Mkuu wa Mkoa(wa nnne kutoka kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA (wa tano kutoka kushoto) pamoja na maafisa wa TAWA na ofisi ya RC mbele ya jengo la Mkuu wa Mkoa

Picha ya pamoja Kati ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu-TAWA(wa tano kutoka kulia) na askari wa Pori la akiba la Lwafi

Mbao zaidi 200 zilizokamatwa zimevunwa na majangili Ndani ya pori la Lwafi
Baadhi ya askari wa pori la akiba Lwafi wakimsililiza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA (haonekani kwenye picha)
Bw. Pascal Mrina aliyesimama, (Meneja. wa Mapori ya Akiba Uwanda na Rukwa-Lwafi)
Dkt. Wakibara akisisitiza Jambo alipokuwa akiongea na watumishi wa pori la akiba  Lwafi(hawaonekani kwenye picha hii)
Askari wa pori la Akiba Uwanda
Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Ng'ombe 319 wamekamatwa Ndani. Ya pori la Akiba Uwanda

Taarifa hii imeandikwa na Bw. Twaha Twaibu (Afisa habari na Mahusiano -TAWA)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search