Miili ya waliouawa DRC yapatikana...soma habari kamili na Matukio360...#share
Jeshi la Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Congo limesema miili ya watu 26 waliouawa katika shambulio
lililofanywa na waasi mapema mwezi huu, imegunduliwa mashariki mwa nchi hiyo.
DRC Congo
Marehemu wote hao
ambao walikuwa ni raia isipokuwa mmoja, walishambuliwa katika eneo la Beni
katika jimbo la Kivu kaskazini wakati wakisafiri na gari ndogo ya kukodi
Mamlaka nchini humo
zinasema kwamba zilishindwa kujua zilipo maiti hizo mapema kwa sababu ya
mapigano makali yaliyokuwa yakitokea katika eneo hilo, ambako mamia ya watu
waliuawa katika siku za hivi karibuni
Jeshi la Congo na
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakililaumu kundi la wapiganaji wa
Uganda la Allied Democratic Forces ADF, kuhusika na mauaji hayo




No comments:
Post a Comment