Takribani watu zaidi 250 wauawa...soma habari kamili na Matukio360...#share


TAKRIBANI zaidi ya watu 250 wameuawa katika mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu, Somalia.

Sehemu ya mabaki ya mlipuko wa mabomu mjini Mogadishu, Somalia
Kufuatia hali hiyo, Rais wa Somalia ametangaza siku tatu za maombelezo.
Hata hivyo uenda idadi hiyo ikaongezeka kutokana na kuripotiwa kuwa wananchi wengi wamejeruhiwa na kukimbizwa Hospitali.

Tukio hilo ambalo limetokea katika ya mji wa Mogadishu limehusisha magari mawali likiwamo lori.

Yote yalikuwa na vilipuzi na yalilibuka katika  mtaa ambao majeshi ya kimataifa(Amisomi) yanaweka ulinzi.

Hadi sasa haijafahamika kundi lililohusika na tukio hilo na kwamba hilo ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.
Tukio hilo linatokea ikiwa ni siku chache baada kujiuzulu kwa waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search