Waziri wa Magufuli avunjiwa nyumba yake....soma habari kamili na Matukio360...#share
NYUMBA ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi imevunjwa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi
Hatua hiyo imetokana na nyumba yake iliyopo katika kijiji cha mapogoro wilayani Isimani mkoani Iringa kunjengwa ndani ya hifadhi ya barabara ya kwenda katika hifadhi ya Ruaha.
Mapema Leo waziri Lukuvi ameiambia Matukio360 kuwa ameshiriki kuvunja nyumba yake na kwamba ni hatua ya kutekeleza maagizo ya nyumba zote zilizowekewa alama ya X, kuvunjwa.
“Navunja nyumba yangu, hivyo nawataka wananchi wenzangu ambao nyumba zao zimewekea X nao wavunje ili kutii sheria na kuunga juhudi za Rais Magufuli kutuletea maendeleo.”
Amesema barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami inafaida kubwa kwa wakazi na nchi kwa ujumla na kwamba kukamilika kwake kutaongeza shughuli za kiuchumi.




No comments:
Post a Comment