Mkurugenzi 'chupuchupu' jela miaka miwili..soma habari na Matukio360..share

Na mwandishi wetu
GULAMABBAS  Murtaza (47) ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Ideal Trading Ltd ya Temeke Chang'ombe  VETA jijini Dar es Salaam, amenusurika kifungo cha miaka miwili jela baada ya kulipa faini ya  milioni 26.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Murtaza amelipa kiasi hicho cha fedha na kukwepa kifungo baada ya kukubali mashtaka mawili ya kuishi bila kibali na kujihusisha  na biashara nchini.

Leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amemuhukumu mshtakiwa huyo kulipa milioni moja katika kosa la kuhishi bila kibali.

Pia  amemuhukumu mshtakiwa huyo kulipa kiasi cha milioni 25  kwa kujihusisha na biashara kama mkurugenzi wa kampuni ya Ideal Trading Ltd iliyopo eneo la Chang'ombe bila ya kuwa na kibali.

Mshtakiwa hiyo alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kukwepa kifungo cha miaka miwili jela.

Mshtakiwa huyo akiwa raia wa India na mkazi  wa  Kenya anadaiwa kufayafanya makosa hayo Oktoba 12, 2017. Upande wa mashtaka uliwakilishwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka Wa Uhamiaji, Novertus Mlay.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search