Naibu Waziri awabana Madiwani...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa  amewataka madiwani  kuanisha vipaumbele vyao vya barabara ili ziingizwe kiurahisi kwenye mpango wa matengenezo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo km 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri,
Ametoa wito huo leo mkoani Tabora alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa km 28 na kuwa  mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.

"Diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukifuatilia hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa",    amesema  Kwandikwa.
Amesisitiza  umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo kutambulika na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa kuwa zitaingizwa katika mipango ya ujenzi kwa wakati.

Kuhusu barabara hiyo ya Kaliua-Urambo inayojengwa kufuatia agizo la Rais Dkt John Magufuli, Kwandikwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora uliopangwa kwa mujibu wa mkataba wake.
"Lengo la mheshimiwa rais ni kurahisha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi hivyo mkandarasi huna budi kufanya kazi hii haraka na kwa kuzingatia makubaliano ya mkataba wako.’ amesema waziri kwandika.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemuhakikishia naibu waziri Kwandikwa kuwa serikali ya mkoa huo imejipanga kushirikiana na mkandarasi ili barabara hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.


“Kwanza sisi kama mkoa tunamshukuru Rais kwa kuona umuhimu wa kutuwekea lami katika barabara hii kwa sababu itaongeza ufanisi kwa wananchi kufanya shughuli zao kiurahisi”, amesema Mwanri.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze amesema kuwa Wakala utawasimamia makandarasi wazawa Samota Construction, Anam Roads Works na Jossam Contractor (JV) ili kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo kwa wakati baada ya changamoto ya tatizo la maji kupatiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri Mhe. Elias Kwandikwa, yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search