Mourinho aendeleza tambo Liverpool vs Manchester United...soma habari kamili na Matukio360..#share



MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amesema litakuwa jambo la kupendeza  kupeleka klabu yake Anfield Jumamosi licha ya kutarajia kutoshangiliwa.




Klabu hizo mbili ni mahasimu wakuu na United wanaweza kuwa alama 10 mbele ya Liverpool iwapo watashinda mechi hiyo ya Jumamosi.

"Tunajua jinsi mashabiki wao waliovyo na uadui dhidi yetu kihistoria, lakini hilo ndilo tunataka," Mourinho amesema.

"Sijawahi kumuona mchezaji akilalamika 'oh, mazingira yalikuwa mabaya sana'."

"Huwa tunalalamika mashabiki wakiwa kimya. Ni jambo la kupendeza kuchezea Anfield. Jambo la kupendeza."

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp atakuwa akiadhimisha miaka miwili Liverpool wikendi hii na atakuwa bila mchezaji wake nyota Sadio Mane.

 Mane aliumia misuli ya paja akichezea Senegal mechi za kufuzu Kombe la Dunia lakini Klopp anaamini wanaweza kujimudu bila yeye.

"Bila shaka bado tunaweza kucheza soka bila Sadio kama tulivyofanya awali - zaidi ya jinsi tulivyotaka," amesema Klopp. "Yeye ndiye mchezaji bora zaidi wetu na ana mkosi sana kuumia.

"Wachezaji wengi wa timu mbalimbali wametoka kuchezea timu za taifa na majeraha - ni tatizo kubwa kutokana na mabadiliko ya mtindo wa mazoezi na uchezaji pia."

"Tunaweza kucheza bila yeye ingawa tungependa sana kuwa na yeye kikosini.

Coutinho kucheza

Liverpool watakuwa bila Mane anayetarajiwa kukaa nje wiki sita, lakini Philippe Coutinho na Roberto Firmino wanatarajiwa kuwepo hata baada ya safari ndefu ya kucheza mechi Brazil.

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini anatarajiwa kutocheza baada ya kuumia kano za goti akichezea Ubelgiji. Nahodha Michael Carrick pia bado anauguza jeraha

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search