Wizara yaomba radhi...soma habari kamili na Matukio360...#share
WIZARA
ya Nishati imeomba radhi kufuatia hatua yake ya kuahirisha mnada wa madini ya Tanzanite
uliokuwa ufanyike katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara kuanzia Oktoba 12 hadi 15, 2017.
Waziri wa madini Angela Kairuki
Taarifa
kwa vyombo vya habari kutoka kitengo cha mawasiliano Serikalini inasema “Wizara
ya Madini inawaomba radhi wadau wote wa
sekta hii ndogo ya madini na vito hususan Tanzanite ambao wameathirika kwa
namna moja au nyingine kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huo.”
Taarifa
hiyo imesema sababu za kuahirishwa ni kuridhia maombi ya wadau wa mnada
walioomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa
wingi.
Pia
uongozi wa Wizara na Mkoa upate muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora
zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Merereni.
Mnada
huo umeahirishwa hadi hapo utapotangazwa




No comments:
Post a Comment