Wa-Oman 300 wawasili Zanzibar.. Soma habari kamili hapa Matukio360.. #share
UJUMBE wa watu 300 ambao wanamwakilisha mfalme wa Oman Sheikh Sultan Qabous bin Said umewasili mjini Zanzibar kwa kutumia meli aina ya ‘ Fulk Al l Salamah' inayotumiwa na familia ya ufalme huo.
![]() |
| Meli ya mfalme wa Oman ikiwaimetia nanga katika Bandari ya Zanzibar |
Ujumbe huo wa Oman uliongozwa na waziri wa mafuta na gesi Mohammed Al-ramh.wa Oman uliongozwa na waziri wa mafuta na gesi Mohammed Al-ramh.
Ziara hiyo inalenga kuhimiza amani na umoja duniani.
Akizungumza katika hafla hiyo, waziri katika ofisi ya makamu wa rais wa pili Mohammed amesema ziara hiyo ni muhimu kwa serikali ya Zanzibar.
Amesema kuwa inafungua ukurasa mpya kuhusu ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili yalio na historia ndefu.
Waziri huyo amesema ujumbe huo pia utapewa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na afisi za serikali ili kubadilishana mawazo kuhusu ukuwaji wa kiuchumi.




No comments:
Post a Comment