Msemaji mkuu wa Serikali atoa siri tano za mafanikio...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Habari
Maelezo na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas ametoa siri tano za mafanikio
kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2017 wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa
mwishoni mwa mwezi huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji mkuu wa Serikali Dk Hassan Abass
Siri ya kwanza ni
malengo ya pili malengo makubwa ya tatu nidhamu na kusimamia malengo, ya nne ushirikiano na siri ya tano
kumshirikisha Mungu kwenye shughuli zote hasa za masomo.
Dk Abbas aliwaasa wanafunzi hao jana alipokuwa mgeni rasmi katika maafari ya 33 ya mwaka 2017
ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne
katika shule ya Sekondari Jitegemee (JKT).
“Siri tano za mafanikio ni lazima ujiwekea malengo hasa makubwa, nidhamu, kujituma, kusimamia malengo
yako, ushirikiano na kumshirikisha Mungu hasa katika masomo yao.”
Dk Abbas amesema mojawapo
ya changamoto inazoikabili shule hiyo vitabu
vya kiada na ziada ameahidi kuwapelekea.
Aliwatunuku vyeti
wanafunzi 459 kati yao wasichana 209 na wavulana 250. Ameahidi kuwa balozi wa shule hiyo.
Akisoma risala kwa
niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne 2017, mwanafuzi Isihaka Jamal alimuomba Dk
Abbas kubuni mfumo wa kuwawezesha wanafunzi kufika shuleni kwa wakati na
kuepukana na changamoto zinazowakabili hasa wanafunzi wa kike.
Jamal alisema
usafiri kwa wanafunzi hasa wakike ni
changsmoto kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakijinasua na tatizo hilo la usafiri
kwa kutafuta njia mbadala kwa kujiingiza katika mapenzi na madereva daladala,
bodaboda na kupelea kupata mimba na magonjwa.
Pia alisema
shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya kuwa majengo mengi ambayo ni ya dhamani,
yanahitaji ukarabati.
Mkuu wa Shule
hiyo ya Sekondari ya Jitegemee(JKT), Luteni Kanali, Robert Kessy aliwaasa
wanafunzi hao kuwa wao wamewaanda kwa kuwapatia elimu bora na nidhamu waizingatie.
Aliwakumbusha
wanafunzi hao kuwa kufika kidato cha nne
siyo wamemaliza masomo hiyo ni elimu
wanatakiwa kuhakikisha wansjiendeleza zaidi kwa kuwa elimu ndiyo ufunguo
wa maisha yao.
Pia aliwaasa
wajiepushe kujiingiza katika matukio ya uhalifu, matumizi ya dawa za kulevya na
vitendo hatarishi
No comments:
Post a Comment