Uteuzi wa Rais Mugabe WHO wapingwa...Soma habari kamili na Matukio360..#share
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO)
limesema linafikiria upya uamuzi wake wa kumteua Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
kuwa balozi mwema wa shirika hilo.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa WHO,
Tedros Adhanon Ghebreyesus.
Hatua hiyo inakuja kufuatia ukosoaji mkubwa kutoka kwa
viongozi mbalimbali ulimwenguni, kutokana na uamuzi huo wa kumteuwa Mugabe anayelaaniwa na watu wengi duniani.
Ghebreyesus, amesema kuwa atatoa taarifa mpya hivi karibuni
kuhusiana na uamuzi huo.
Kwa upande wa serikali ya Uingereza ikizungumzia hatua ya WHO
kumteua Mugabe kuwa balozi, imesema, imeshtushwa na kuvunjika moyo juu ya
uteuzi huo.
Msemaji mjini London, ameleza kuwa bwana Mugabe anakabili
vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya, na kuteuliwa kwake, kutaathiri kazi za
WHO.
Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo , Mkurugenzi mkuu mpya wa WHO,
Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya
umma.
Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka thelathini
na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo
wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara , na kumekuwa na ukosefu
mkubwa wa dawa muhimu .
Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza
kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile
kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.
No comments:
Post a Comment