Mwalimu ajiua kwa kujichinja koromeo...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
Leonard Mwipugi (29) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari
ya Mtenga wilayani Nkasi, amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio Mratibu wa Elimu Kata ya
Mtenga, Hebron Mwafungo amebainisha kwamba Mwipugi amekutwa akiwa amekufa baada
ya kujichinja.
Amefafanua kuwa marehemu amafanya kitendo hicho nyumbani
kwake jana saa sita mchana.
Aidha Mwafungo amesema kabla ya mwalimu huyo kukutwa amejiua,
alikwenda kazini kwake na saa 5 alirejea nyumbani ambapo hakumkuta mkewe.
Ameelza baada ya muda
walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo
akiwa chumbani kwake.
Amebainisha kwamba licha Mwipugi kuishi na mkewe alikuwa pia akiishi
na mdogo wake na wakati wa tukio hilo alikuwa
amemtuma mbali kidogo ya nyumbani.
Hivyo baada ya mdogo huyo kurudi aliona damu zikichuruzika na
alipochungulia chumbani alikuta kaka yake amekwishafariki.
No comments:
Post a Comment