Zitto ampa 'tano' Nyalandu, katibu wa Bunge anena...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
SAA chache baada ya aliyekuwa
mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kujiuzulu ubunge na nafasi zake zote CCM, mbuge wa
Kigoma mjini, Zitto Kabwe na katibu wa Bunge Stephen Kigaigai wamezungumzia suala hilo.
Spika wa Bunge, Job Ndugai kulia akiwa na Katibu mpya wa Bunge, Stephen Kigaigai wakibadilishana mawazo mara baada ya kuapishwa kwake hivi karibuni Ikulu jijini Dar es Salaam
Kwa nyakati tofauti wamezungumzia suala hilo huku Zitto ambaye pia ni kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo amempongeza kwa uamuzi wake huo.
Katika ukarasa wake
wa tweeter Zitto ameandika “Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki
za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa Nchi unavyoporomoka.”
Hata hivyo katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema bado ofisi yake
haijapata barua rasmi ya kujiuzulu Ubunge kwa Nyalandu
Kagaigai ameiambia Matukio360 kuwa ofisi yake bado haijapokea barua rasmi ya kujiuzulu Ubunge kwa Nyalandu.
Leo
jijini Arusha akitangaza uamuzi huo, Nyalandu amesema ‘nimeamua kujiuzulu
nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama
kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
‘Halikadhalika,
asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge,Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu
nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM,
nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa
kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.’
Amesema
uamuzi wake huo ni kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa
ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma
wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi
kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji
kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru
uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.
VILEVILE,
Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya
kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea
kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la
Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na
wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
MIMI
Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia
ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa,
Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa
mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM
imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali.
AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama
kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine,
CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na
kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU
Julius Kambarage Nyerere.
Hivyo
basi, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya
KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba
IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi
waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na
watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa
kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
VILEVILE,
nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu
kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI
wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini
Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu
niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye
mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa
Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote
ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane kisera na
kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na
nchi yenye MAADILI.
No comments:
Post a Comment