Picha Za Unyanyasaji wa Kingono kwa Watoto Zatakiwa Kutolewa Taarif Ziweze Kuondolewa....Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
TAASISI ya kutetea watoto ya C-SEMA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini wamefungua dirisha 'portal' kwa ajili ya picha zinazohusu matukio ya watoto, zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto, kuondolewa katika mitandao ya kijamii.
Meneja wa huduma wa simu ya mtoto wa C-SEMA, Thelma Dhase akizungumza
juu utoaji wa taarifa zinazohusiana na picha za unyanyasaji wa kingono
kwa watoto kuweza kuondolewa katika kulinda watoto wengine leo jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza katika ufunguzi wa dirisha, Meneja Huduma wa Simu ya Mtoto , Thelma Dhase amesema kuwa picha za matukio za ukatili wa watoto hazitakiwi kuendelea kusambaa katika mitandao.
Amesema kuwa mfumo huo umeanza nchini lakini mradi huo unafanywa duniani nchi 18, ambapo kwa Afrika Tanzania ni ya Nne kuwa na mpango huo katika kutoa taarifa za picha za unyanyasaji wa kingono katika mitandao.
Dhase amesema kuwa mradi huo utasaidia kuongeza usalama wa watutmiaji wa mitandao kuhakikisha watoto waliothirika na picha za unyanyasaji wa kingono hawapitii unyanyasaji zaidi katika mitandao ya kijamii.
Kwa upande wa Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Semu Mwakyanjala amesema picha za watoto zinaonesha ukatili au udhalilishaji wa watoto, hazitakiwi kusambazwa katika mitandao ya kijamii na mtu akipata picha hizo anatakiwa kutoa taarifa ziweze kutolewa katika mitandao.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA),
Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa
watumiaji wa mitandao kutoa taarifa juu ya picha za unyanyasaji wa
kingono kwa watoto iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwakyanjala amesema picha zinazodhalilisha watoto hazitakiwi kutokana na picha hizo zitaawathiri kisaikolojia wakishakuwa watu wazima.
Mradi wa kutolea taarifa za unyanyasaji wa kingono kwa watoto unaendeshwa na Internet Watch Foundation ambao unatekelezwa nchi 18 duniani.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment