Watanzania watahadharishwa kuhusu Bangi...soma habari kamili na Matukio360...#share



SERIKALI wilayani Chunya mkoani Mbeya imewataka wananchi kuacha kuendeleza shughuli za  kilimo cha bangi na badala yake walime mazao ya biashara na chakula.

 








Mkuu wa wilaya  hiyo Rehema Madusa ameimbia Matukio360 kuwepo kwa taarifa za watu wachache

kuendeleza kilimo cha bangi katika baadhi ya mashamba na misitu iliyopo wilayani humo.



“Kata ya Matwiga ni mojawapo ya maeneo ambayo kilimo cha bangi kinaendelea, hii inatokana na baadhi ya viongozi kuwaficha kwa maslahi yao,” amesema



Amesema pamoja na changamoto hiyo atashirikiana na wananchi waadilifu kuwabaini wanaondeleza kilimo hicho



"Wananchi ndio wanaotambua mienendo ya wakulima na wale  wanaolima bangi,  sasa watoe ushirikiano kwa Serikali.  Bangi ni mojawapo ya

madawa ya kulevya hivyo hatuwezi kukubali vizazi viharibike.”



Pamoja na mambo mengine  Madusa ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama wilaya humo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.



Ofisa Mtendaji kata ya Matwiga, Moses Rudisha amethibitisha kuwapo kwa hali hiyo na kwamba changamoto ni  namna ya kuwafikia kutokana na umbali  wa maeneo  inapolimwa bangi.



 "Katika kata hii bangi inalimwa kwa vificho na kwenye mapoli pia miundombinu ya huku si salama na rafiki."amesema.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search