Waziri Mpina asema Serikali kudhibiti uvuvi haramu...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kusimamia sheria za uvuvi ili kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vinavyosababisha kutoweka kwa baadhi ya viumbe vya majini.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kusimamia sheria za uvuvi ili kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vinavyosababisha kutoweka kwa baadhi ya viumbe vya majini.
Baadhi ya washiriki wa kongamano
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Waziri Mpina wakati akifungua kongamano la siku nne kwa niaba Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan linalokutanisha Wanasayansi wa Bahari kutoka Ukanda
wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) linalojadili masuala mbali mbali
yanayohusu shughuli za Baharini.
Ameeleza kuwa baadhi ya viumbe vya
baharini vimekuwa vikitoweka kutokana na shughuli za binadamu kama za uvuvi
haramu pamoja na utililishaji wa maji ya sumu baharini.
“Uvuvi haramu, utililishaji wa maji
ya sumu kutoka viwandani haya yanachangia kupotea kwa viumbe baharini, ndio
maana tumekutana kwenye mkutano huu kujadili ili tuweze kutafuta ufumbuzi wa
tatizo hili,” amesema Mpina.
Amesema katika mkutano huo wadau
watajadili mikakati ya namna ya kusaidia kuondokana na changamoto za uvui
haramu pamoja utumiaji wa utilishaji wa kemikali hizo akitolea mfano kemikali
hatari ya Zebaki.
“Serikali tutachukua haya
mapendezeko yote yatakayotolewa na wadau hawa ili ziweze kuchukuliwa kuondokana
na hizi changamoto”amesema Mpina.
Kwa wake Mkurugenzi wa wa Taasisi
ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini,Profesa Yunus Mgaya ameishauri serikali
kusimamia sheria zake ili kuweza kudhibiti vitendo haramu vya uvuvi.
Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini,Profesa Yunus Mgaya.
“Sheria zipo naishauri serikali itilie
mkazo wa nguvu kwenye sheria za uvuvi haramu ambapo itachangia kupunguza
vitendo hivi”ameishauri Profesa Mgaya.
Mkutano huo wa siku nne umeanza
leo Oktoba 30,2017. Utamalizika Novemba 4, 2017,umekutanisha wadau mbali mbali kutoka nchi tofauti .
No comments:
Post a Comment