Watoto 7500 wakosa elimu...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
mwandishi wetu
TAKRIBANI
watoto 7500 wa kati ya umri miaka mitano na 15 wa Tarafa ya Kipembawe wilayani
Chunya mkoani Mbeya wanatumikishwa ikiwamo kuchunga mifugo na kulima
Mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akiwa katika moja ya mikutano
Hali
hiyo imepelekea kukosa fursa ya kusoma kutokana na wazazi kutoka mikoani
kujikita zaidi katika shughuli za kilimo
na ufugaji kinyume cha sheria.
Akizungumza
na Matukio 360 Mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa amesema idadi hiyo
imegundulika Oktoba 7,2017 baada ya kufanya oparesheni ya kuwaondoa
wakulima na wafugaji waliovamia maeneo ya misitu na hifadhi.Jumla ya kaya 1,500
ziliteketezwa.
Amesema
kutokana na idadi hiyo serikali itawachukulia hatua za kisheria wazazi waliokataa
kwa makusudi kuwapeleka shule watoto wao
“Idadi hii imenishtua nimewaangiza watendaji
na wenyeviti wa vijiji kufanya kila
linalowezekana
kuhakikisha ifikapo Januari, 2018 wanaanza masomo,’ amesema
Pamoja na mambo
mengine Madusa amesema Serikali imelazimika kufanya oparesheni hiyo
baada ya kubaini uharibifu mkubwa
wa mazingira ,ujenzi holela wa makazi hususan kukosekana kwa huduma muhimu
kama shule, zahanati, maji safi
na salama na nishati
ya umeme.
Ofisa Mtendaji wa
Kijiji cha Mbuzi, Nicolaus Ndugusa, amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na
kwamba sababu ni mwamko duni wa kutotambua umuhimu wa elimu.
Mkulima, Mathias
Shuma amesema sababu ya kutowaandikisha watoto shule ni mila na desturi
walizojiwekea ya kuwa mtoto akipata elimu hatosaidia wazazi na kuhudumia mifugo.
No comments:
Post a Comment