TWAWEZA: Asilimia 67 wanataka katiba mpya...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya TWAWEZA imesema asilimia 65 ya watanzania wanataka katiba mpya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti waliofanya juu ya Katiba Mpya jijini Dar es Salaam
Wakati utafiti huo wa Twaweza ukionyesha wananchi wengi wakidai Katiba Mpya Rais John Magufuli amesema kwa sasa Katiba mpya sio kipaumbele
cha serikali yake .
Twaweza inayohusika na
masuala ya utafiti nchini inaeleza kuwa asilimia
67 ya wananchi nchini wanataka katiba mpya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Aidan Eyakuze amesema utafiti wao uliitwa ‘Zege imelala?’ Maoni ya wananchi kuhusu kukwama kwa
mchakato wa kuunda katiba mpya.
Amesema utafiti huo unatokana na takwimu za sauti ya
wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia
simu za wananchi ambapo amefafanua matokeo hayo yanatokana na takwimu
zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,745 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara
mwezi Juni hadi Julai mwaka huu.
“ Wananchi wanataka Katiba mpya. Wengi wao wanataka mchakato uanze
upya na tume mpya katika ukurasa mpya. Hata hivyo, wapo wananchi amabo wapo
tayari kusonga mbele kwa kutumia rasimu iliyoandaliwa na tume iliyotangulia,”
amesema Eyakuze.
Aidha katika utafiti huo Eyakuze amesema asilimia 56 wametaka
toleo la mwisho la rasimu ya katiba lipigiwe kura na wananchi huku asilimia ya
48 ya wananchi wakabainisha kuwa Katiba mpya haitapatikana ndani ya miaka
mitatu ijayo.
Amebainisha, wananchi wameendelea kuunga mkono kwa nguvu
uundwaji wa katiba mpya inayotilia mkazo suala la uwajibikaji ambapo asilimia
79 wanataka mawaziri wawe na uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya chaguzi
iwapo hawatatekeleza majukumu yao ipasavyo.
Hata hivyo Eyakuze ameeleza kwamba wananchi wamegawanyika
kwenye baadhi ya hatua katika uwajibikaji zilizopendekezwa ikiwemo kuzuia viongozi na
watumishi wa umma kuwa na akaunti nje ya nchi ambapo asilimia 52 wanaunga mkono
kuwepo kwa ukomo wa ubunge , asilimia 52 wanaunga mkono na kuweka kanuni za
uwazi na uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu ya Taifa.
Aidha wananchi wanaunga Mkono kuondolewa kwa kipengele
kinachotaka kuchunguza na kudhibiti Ofisi ya Rais ambao ni asilimia 56 pamoja
na mawaziri kuchaguliwa nje ya bunge asilimia 62.
Akizungumzia muundo wa serikali unaotakiwa katika katiba hiyo
mpya Eyakuze amesema asilimia 42 ya wananchi waliunga mkono muundo wa serikali
mbili huku muundo wa serikali moja ukiungwa mkono kwa asilimia 25 wakati wa
serikali tatu ukiwa kwa asilimia 16.
Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole
akichangia maoni yake juu ya utafiti huo, amesema hana shaka na utafiti huo,
lakini amesisitiza kuwa pamoja na kutakiwa kwa katiba mpya cha muhimu ni
viongozi waliopewa dhamani kuiishi katika katika kuwatumikia wananchi.
Naye Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Deogratius Bwire
amesema kuwa cha muhimu ni kuwa na Katiba mpya iliyoandikwa ili mwananchi awe
na haki ya kudai kitu ambacho kimo ndani ya katiba kwani Katiba ndiyo mfumo
mzima wa mwongozo wan chi.
No comments:
Post a Comment