Waziri Kalemani azibana kampuni za mafuta..soma habari na Matukio360...#share

Salha Mohamed
SERIKALI imezitaka kampuni za kuhifadhi mafuta (Tiper) na Puma kutoa taarifa za shughuli wanazofanya kila baada ya miezi mitatu.
Hatua hiyo imefikiwa kutokana na kampuni hizo kutotoa taarifa za shughuli zao ikiwamo mapato serikalini.
Meneja bohari kutoka kampuni ya puma, Auni Yeteri  akimuonesha Waziri wa Nishati,  Dk. Medard Kalemani matanki ya kuhifadhia mafuta alipofanya ziara katika kampuni hiyo Kurasini jijini Dar es Salaam Leo
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati  Dk Medard Kalemani na kwamba  serikali inaziangalia kampuni hizo kwa macho ya ndani na kuangalia shughuli wanazozifanya za kiutendaji kila baada ya miezi mitatu.
“Katika makampuni haya Serikali ina hisa ya asilimia 50 kupitia msajili wa hazina na  hazijawahi kutoa taarifa ya shughuli zao serikalini.” Amesema na kuongeza “Hivyo kila baada ya miezi mitatu mnatakiwa kuleta ripoti zenu serikalini ikiwamo za mapato.”
Amesema kutaka taarifa hizo ni serikali kutaka kujua kinachoendelea na kinyume na hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia  ameyataka makampuni hayo kumaliza ukarabati wa matenki ya kuhifadhia mafuta ndani ya wiki moja.
"Kampuni ya Puma haijafika mikoa  sita nchini, sasa mfungue vituo mikoa yote hadi kufika mwakani ili msilalamikie mapato mkifika mikoa yote itasaidia kuongeza mapato kwa sababu mahitaji yapo...ikifika Januari mwakani nitafuatilia."amesema
Amesema kwa sasa Wizara yake imeweka dawati maalumu la kufuatilia Puma hivyo wajitahidi kutatua changamoto za kampuni hiyo na kuwataka wafanyakazi kuwa wazalendo na kuacha kushirikiana na walinzi kuiba mafuta.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Puma, wamesema kumekuwa na changamoto ya meli kushusha mafuta kwa siku 10 badala ya siku 5 jambo linalosababisha wakati mwingine vituo kukosa mafuta.

Kwa upande wake Msaidizi wa Mkurugenzi Kampuni ya Tiper, Paulo Mzava amesema kampuni hiyo imechangia asilimia 68.5 ya mapato serikalini huku ikiwa imeagiza Flow mita sita ili kuongeza mapato zaidi

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search