'Updates' kutoka anapohojiwa Zitto Kabwe atuhumiwa kwa makosa mawili...soma habari kamili na Matukio360..#share

 Na mwandishi wetu
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, anaendelea kuhojiwa  na Polisi  katika kituo kikuu cha Chang'ombe  wilayani Temeke jijini dar es salaam akituhumiwa kufanya makosa  mawili ya uchochezi.
  

Zitto Kabwe
Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamis ameiambia Matukio360 kuwa katika mahojiano hayo, Zitto ameambata na  timu ya wanasheria wa chama hicho akiwamo wakili Steven Mwakibola na Venas Msebo.

Miongoni mwa makosa anayoojiwa ni kwamba Jumapili ya  Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:

1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.


2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search