Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amewataka Wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa  kuzingatia vigezo kumi vilivyomo kwenye hati maalum ya rais.
Pix 01
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam akizindua Bodi hiyo, ametaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na  malipo ya mishahara na masilahi kwa watumishi hao yanapatikana na kuwa endelevu, kuhakikisha utumishi huo unavutia na kubakiza taaluma zinazohitajika katika kuendeleza shughuli zake, utendaji wenye tija uanatambuliwa pamoja na uwazi,usawa na haki zinazozingatiwa.

Aidha Bodi hiyo ameikabidhi  miongozo, taratibu na sheria zinazotakiwa kufuatwa wakati ikitekeleza majukumu yake.

Amesesma endapo bodi hiyo itazingatia vigezo hivyo itajenga imani kwa watumishi wa umma na wadau wenginge huku akisisitiza kinyume ha hapo itashindwa kufanya yake ipasavyo hali itakayosababisha kutokidhi matarajio ya Serikali, watumishi hao, wadau wengine ambao ndio watoaji masilahi hayo kupitia kodi.

"  Ni wazi kwamba, endapo mtazingatia vigezo hivyo ushauri mtakaoutoa mara kwa mara utakuwa ni usahauri bora na wenye manufaa makubwa kwa taifa letu kwa hali hiyo mtajenga imani kwa watumishi na wadau wengine," amesema waziri Kairuki.

Amebainisha kuwa Serikali itatoa ushirikiano kwa bodi hiyo katika kuhakikisha masilahi ya watumishi hao yanaboreshwa ili kuongeza tija huku akitilia mkazo changamoto zilizoisumbua bodi ya kwanza zimeanza kupungua hasa hasa suala la ushirikiano na taasisi za umma.
Pix 03
Amevitaja vigezo vingine ni malipo yanayostahili, yanayolipika na endelevu yanayotolewa kwa ngazi zote katika utumishi huo ili kuvutia na kubakiza vipaji maalum, matakawa ya mlipa kodi ya umma na umma kwa ujumla yanapewa kipaumbele dhidi ya masuala ya mengine wakati wa kubuni na kuendesha vyombo vya masilahi, vigezo katika kupanga masilahi ktatika utumishi huo vizingatiwe kuepuka upendeleo, kuhakikisha viwango vya malipo havitofautiani isipokuwa kwa kuruhusu tofauti kutegemea aina ya kazi na majukumu, maamuzi kuhusu mishahara na masilahi unazingatia hali ya soko la ndani na kikanda pamoja  na kuepuka aina yoyote ya ushawishi wa kisiasa katika maamuzi yanayohusu mishahara na masilahi ya wataumishi.

Mwenyekiti wa bodi hiyo ni Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula, Katibu Mkuu Mstaafu Balozi Charles Mutalemwa(Makamu Mwenyekiti), Katibu Mkuu wa Bunge Mstaafu George Mlawa (Mjumbe), Waziri Mstaafu Gaudensia Kabaka(Mjumbe), Jaji Mstaafu Regina Rweyemamu (Mjumbe), Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawii(Mjumbe) na Kamishna Mwandamizi wa Polisi Mstaafu, Jamal Rwambow (Mjumbe).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa hiyo, Ndagula alimshukuru rais kwa kuiteua bodi huku akiahidi kutekekeleza majukumu yote yaliyoanishwa kwa kuzingatia weledi na maadili ya utumishi wa umma.
Pix 05

Na Hussein Ndubikile

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search