Waziri Lukuvi awapa mtihani Wakurugenzi, Maafisa Ardhi, Ujenzi na Mipango miji..Soma habari kamili na Matukio360..#share

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (katikati) akisoma nyaraka.

Aidha ameagiza pia kuvunjwa majengo yaliyojengwa katika viwanja vya watu wengine kwa kumiliki  hati za ardhi kwa dhuruma.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa kwa lengo la kutatua mgogoro wa ardhi katika shamba la mifugo lenye ukubwa wa ekari 12,750.

Ametaka shamba hilo lirejeshwe serikalini kwa kuwa utaratibu wa kuligawa umekiukwa kwa kiwango kikubwa huku  masharti ya uendeshaji yakiwa hayajazingatiwa.

Amesema tatizo la ujenzi holela huchangiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipango miji ambao wanaacha majengo yanajengwa katika miji yao bila kujua ujenzi huo umefuata taratibu.

“Hatuwezi kuendelea na zoezi la kufanya urasimishaji wa makazi kila siku wakati chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyo naagiza Wakurugenzi, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka X katika majengo yote yanayojengwa bila vibali na ujenzi unaofanywa kwenye viwanja vya watu masikini kwa dhuruma” amesema Lukuvi.
Lukuvi amesema atapambana na viongozi hao pale ambapo atakuta majengo yamekithiri katika miji yao na hayana vibali vya ujenzi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemhakikishia Waziri Lukuvi kuwa atayafanyia kazi mapendekezo yake kikamilifu na kwa haraka ili kuondoa migogoro na kero zinazoukabili mkoa wake katika masuala yote ya ardhi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search