Ajali 1375 zatokea Julai hadi Septemba...soma habari kamili na Matukio360..#share

Salha Mohamed
JESHI la Polisi kikosi cha usalama barabarani limesema ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 48 ukilinganisha na mwaka 2016 na ajali 1375 zimetokea kati ya Julai na Septemba 2017.

Kamanda wa polisi kikosi cha Usalama barabarani, Fortunatus Musilimu akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika katika viwanja vya biafra kuanzia Novemba 18 hadi 25, 2017.

Kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani, Fortunatus Musilimu amesema hayo  jijini Dar es Salaam kwenye  uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama itakayoanza Novemba 18 hadi 25, 2017 katika viwanja va Biafra na kuwa takwimu hizo ni za nchi nzima.

Amesema ajali hizo zimesababisha vifo vya watu 625, majeruhi 1486 ukilinganisha na mwaka 2016 katika kipindi kama hicho kulikuwa na ajali 2639, vifo 923 na majeruhi  2460 ambapo takwimu zinaonesha upungufu wa ajali ni 1264 sawa na asilimia 48, upungufu wa vifo 298 sawa na asilimia 32 huku pungufu ya majeruhi ikiwa 974 sawa na asilimia 40.

 “Kabla ya kuanza maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Kilimanjaro kuanzia Oktoba 9 hadi 15, 2017 kulikuwa na ajali 46, vifo 56 na majeruhi 35 …wiki ya maadhimisho ya usalama wa barabarani kuanzia Oktoba 16 hdi 22 mwaka huu kulitokea ajali 37 vifo 48 na majareruhi 32,”amesema.

Amesema kutokana na takwimu hizo na kutoa elimu ya usalama barabarani wamepunguza ajali 9 sawa na asilimia 20, vifo 8 sawa na asilimia 14 na majeruhi 3 sawa na asilimia 7 na kuwa maadhimisho hayo yamesaidia.

Amesema takwimu za maadhimisho yaliyofanyika Septemba 26, hadi Oktoba 2,2016  kulitokea ajali 50, vifo 49 na majeruhi 42 ukilinganisha na maadhimisho yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro kuanzia Oktoba 16 hadi 22, 2017 kulikuwa na ajali 37 vifo 48 na majeruhi 32.

Ameishukuru benki ya stanbic kwa kutambua juhudi ambazo wanazifanya katika kukabiliana na ajali za barabarani nakuhakikisha elimu inatolewa kwa watu wengi na kwa muda mfupi ili kusasaidia kuokoa maisha ya watanzania.

Amewataka madereva kutii sheria bila shuruti na watachukulia hatua kali za kisheria madereva wazembe

Kwa upande wake mkuu wa matawi na mitandao wa Benki ya Stanbic, Musa Kitoa amesema lengo lao ni ifikapo mwaka 2020 ajali zipungue hadi asilimia 50.

“Tutatoa elimu kwa watu wengi, tutatengeneza video, stika atakayeona usalama barabarani si mzuri apige simu kuwajulisha wahusika, tumeandaa watu kwa ajili ya kutoa alimu kwa madereva wa magari yanayobeba wanafunzi,”amesema.

           


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search