Askofu ampa 'tano' Magufuli...soma habari kamili na Matukio360..#share
Salha Mohamed
MWENYEKITI wa taasisi
ya Good News for All Ministry, Askofu Dk Charles Gadi amempongeza rais Dk John
Magufuli kwa kusimamia rasilimali za nchi na kurejesha malimbikizo ya kodi.
Mwenyekiti wa taasis ya Good News For All Ministry Dk. Charles Gadi (katikati) akiendesha maombi ya kuomba mvua isilete madhara kwa jamii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mchungaji James Mwageni, kulia ni Mchungaji Palemo Massawe.
Pongezi hizo amezitoa
leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari lengo likiwa ni
kuomba mvua zinazonyesha zisilete maafa kwa wananchi na kumpongeza rais kwa
juhudi za kusimamia ipasavyo rasilimali za nchi.
Amesema rais
amefanikiwa kusimamia eneo la madini ya dhahabu na vito kwa kiwango cha
kuwezeshwa kurudisha sehemu ya malimbikizo ya kodi ambayo kwa namna moja au
nyingine huenda zisingerudishwa.
“….tusingezipata
kama si msimamo wake wa kutoyumba dhidi ya makampuni ya madini . Ni habari za
kufurahisha ingawa bado taifa linategemea malipo mengi zaidi kutoka kwa
makampuni hayo,”amesema.
Amesema
hatua hiyo ya sasa ni msingi mkubwa na imara ambao umewekwa na rais Magufuli na
kwamba kwenye vito vya thamani kama Almasi, Tanzanite kuna mengi ambayo nchi
itafaidika nayo.
Katika
hatua nyingine, ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA) kwa tahadhari ya
uwezekano wa kuwepo kwa mvua itakayoleta madhara kama itanyesha kwa kiwango
kilichotabiriwa.
“Hii
ni hatua ya maendeleo kiteknolojia kwa idara hiyo, jambo linalowawezesha wale
wanaoishi kwenye maeneo hatarishi kuweza kuchukua tahadhari mapema ili kulinda
maisha na hali zao,”amesema.
Amesema
wao huamini kuwa mvua za Mungu hazileti madhara kwa watu, kwani alishaapa baada
ya gharika ya Nuhu hata iangamize dunia
kwa maji.
No comments:
Post a Comment