HALIMA MDEE: Hatutakaa kimya kuhusu Tundu Lissu...soma habari kamili na Matukio360..share
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kawe, Halima
Mdee amesema Chadema kamwe haiwezi kukaa kimya kuhusu tukio la kushabuliwa kwa risasi mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu.
Mbuge wa Kawe, Halima Mdee
Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha Televisheni nchini, na kwamba wanaodai kuwa chama hicho kimeishiwa sera kwa kulifanya tukio hilo kama agenda wana hoja nyepesi.
Amasema tukio hilo ni zito ambalo lingeweza kutoa uhai
wa kiongozi huyo, hivyo chama kitaendelea kulisema hadi hapo vyombo vya usalama vitakapo chukua hatua stahiki dhidi ya wahusika.
Amesema jambo kubwa linalowasukuma kupaza sauti dhidi ya kitendo hicho ni kutokana na Lissu kufanyiwa unyama huo katika eneo ambalo linaaminika liko salama.
Mdee amebainisha kuwa hawafanyi hivyo kwa ajili ya kutafuta 'kiki' na kuvitaka vyombo
vya usalama kuhakikisha vinawakamata waliofanya shambulio hilo.
"Hatuwezi kukaa kimya kwa matukio yanayotokea, huu siyo
utamaduni wetu. Siyo utamaduni wetu watu kupotea bila jeshi la polisi kutoa
taarifa inayoeleweka, viongozi kutolewa silaha hadharani na watu ambao
wanaaminika wanajulikana lakini hatujaona wakichukuliwa hatua,”
“Mbunge kupigwa risasi maeneo yenye CCTV kamera na waliofanya
tukio hilo kutokamatwa, Wananchi kuchanga fedha kwa ajili ya maafa na kisha
kutumiwa kwa kazi nyingine na serikali au ni kiki ipi ambayo tunaitumia au kiki
ni nini wakati tunakemea mambo yanayohatarisha ulinzi na Usalama?," amehoji
Mdee.
Amesema kama ni sera, Chadema bado kina sera ambazo wanaendelea kuzitekeleza ikiwemo walizoahidi wakati
wa uchaguzi na kwamba kama chama hawawezi kushindwa kuwa na sera lakini ni
lazima wakemee mambo ambayo awali hayakuwahi kuzoeleka na kuonekana nchini.
No comments:
Post a Comment