Tafiti za kisayansi hupunguza magonjwa kwa asilimia 40...soma habari kamili na Matukio360..#share
Salha
Mohamed
IMEELEZWA
tafiti za kisayansi zikitumika vizuri hupunguza asilimia 40 ya magonjwa kwa
binadamu
Katibu wa Chama cha watoa huduma za afya binafsi Dk. Rebeca John (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la nne la kitaifa la afya, katikati ni Rais wa chama hicho Dk. Omary Chillo na kulia ni Afisa Tawala wa chama hicho Joseph Mhagama.
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na taasisi ya Tanzania Health Summit
inayoratibu kongamano la Afya nchini, lengo likiwa kujadili changamoto za afya
na kuboresha sekta hiyo.
Kongamano
hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 14 na 15, 2017 katika Ukumbi wa kimataifa za Mwalimu Nyerere(JNICC),
litajadili juhudi za serikali na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi
katika afya.
Kiongozi
wa kongamano hilo, Dk Omary Chillo amesema mapendekezo yanayoonesha suluhisho yatatolewa na kuandikwa
vitabuni na kusambazwa kwenye taasisi za
afya na utekelezaji wake utafuatiliwa.
Amesema
wanatarajia kupata wadau wa Afya takribani 500 kutoka ndani na nje ya nchi
wakiwemo wataalamu wa Afya, watunga sera, watafiti wa magonjwa, wachumi,
wazambazaji wa vifaa tiba na dawa, wawekezaji katika sekta ya Afya na wadau
wote wa sekta hiyo.
Amesema
watafiti mbalimbali watajadili na kutoa majibu ya tafiti zao kama walizofanya
kwa panya kugundua magonjwa ambapo tafiti hizo zikitumika vizuri mtu anauwezo
wa kujikinga na magonjwa kwa asilimia
40.
Kwa
upande wake Katibu wa Taasisi hiyo,Dk Rebecca John ametoa wito kwa wadau wa
afya kutoka Serikalini, mashirika binafsi, hospitali, Asasi zisizo za kiserikali,taasisi
za kitaalamu, watengenezaji wa bidhaa za afya, wazambazaji, wawekezaji na
washiriki wa maendeleo kushiriki katika mkutano huu.
Kauli
mbiu ya mkutano huo ni ‘Ni jinsi gani tunaweza kufikia malengo ya kuimarisha
upatikanaji wa afya bora kwa kuunganisha tafiti za kisayansi, ubunifu na sera
za afya huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mganga Mkuu wa Seriakali, Profesa
Hashim Kambi.




No comments:
Post a Comment